2ndNeoac
That’s right, we encourage organic 100%
+255 (767) 625 264

Press Release

KONGAMANO LA PILI LA KITAIFA LA KILIMOHAI KUFANYIKA MKOANI DODOMA, OKTOBA, 2021

DAR ES SALAAM, 09 JULAI, 2021: WIZARA YA KILIMO WAKISHIRIKIANA NA WADAU WA KILIMO WAKIWEMO SHIRIKA LA MPANGO WA CHAKULA LA UMOJA WA MATAIFA (FAO), TAASISI YA KILIMO ENDELEVU (SAT), SHIRIKA LA SWISSAID, CHUO CHA KILIMO CHA SOKOINE, ASASI YA KILIMO YA ISLAND OF PEACE, SHIRIKA LA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA LA KIJERUMANI (GIZ), MTANDAO WA BIONUAI WA TANZANIA (TABIO), ST. JOSEPH SUSTAINABLE NA TAASISI NYINGINE ZA KILIMO, WAMEANDAA KWA MARA YA PILI KONGAMANO LA KITAIFA LA KILIMOHAI (2ND NATIONAL ECOLOGICAL ORGANIC AGRICULTURE CONFERENCE) LINALOTARAJIWA KUFANYIKA MKOANI DODOMA, TAREHE 21 NA 22 OKTOBA, 2021.

MADHUMUNI LA KONGAMANO HILI LA PILI NI PAMOJA NA KUPATA MREJESHO WA MAADHIMIO TULIYOJIWEKEA KWENYE KONGAMANO LA KWANZA LA OKTOBA, 2019, YAKIWEMO KUANZISHWA KWA DAWATI LA KILIMOHAI KWENYE WIZARA YETU YA KILIMO; LAKINI PIA KITUO CHA UTAFITI CHA BIHAWANA DODOMA, KUTOA MAFUNZO NA MBINU ZA KILIMOHAI; NA MENGINEYO.

PAMOJA NA MREJESHO HUO, MWAKA HUU SERIKALI PAMOJA NA WADAU WA KILIMOHAI TUNATARAJIA KUTENGENEZA MKAKATI WA KILIMOHAI YAANI ORGANIC AGRICULTURE STRATEGY AMBAYO ITAELEZEA UTEKELEZAJI WA MASWALA YA KILIMOHAI KATIKA SERA YETU YA TAIFA YA KILIMO. MCHAKATO HUU UTAANZA SIKU CHACHE ZIJAZO NA KUJUMUISHA WAWAKILISHI WATAALAMU KUTOKA SERIKALINI, AKADEMIA NA ASASI ZA KIRAIA ZA KILIMO.

KILIMOHAI NA WAKATI MWENGINE UFAHAMIKA KAMA KILIMO IKOLOJIA NI KILIMO KISICHOTUMIA KEMIKALI ZA VIWANDANI KINACHOZINGATIA UZALISHAJI UNAOMLINDA MLAJI, UDONGO NA MAZINGIRA. KAMA INAVYO FAHAMIKA, MAGONJWA YA MILIPUKO NA YALE YASIOAMBUKIZWA YAANI NON-COMMUNICABLE DISEASES NDIO CHANZO KIKUBWA CHA VIFO DUNIANI. NA MAGONJWA HAYA KWA ASILIMIA TAKRIBAN 99 UTOKANA NA MAISHA TUNAYOISHI LAKINI ZAIDI VYAKULA TUNAVYO KULA VILIVYOJAA KEMIKALI ZINAZOTOKANA NA PEMBEJEO ZA VIWANDANI ZINAZOTUMIKA KWENYE MASHAMBA YETU AU MAGHALA YETU YA KUIFADHIA CHAKULA.

UTAKUTA KWA MFANO MATUNDA MENGI YANAYOUZWA KWENYE BARABARA ZETU YANAKAA JUANI ZAIDI YA WIKI MBILI BILA KUHARIBIKA. HIZO NI KEMIKALI TUPU ZINAZOTUMIA KUYALINDA. NA JE, USALAMA WAKE KWA MLAJI UPOJE? BAADHI YETU TUNAJILIMIA BUSTANI ZETU NYUMBANI NA ZINAZOTUSAIDIA KUJUA NI KITU GANI TUNA KULA AU TUKILAZIMIKA KWENDA SOKONI, TUNANUNUA MBOGA KAMA KABICHI ZILIZO NA MATUNDU KUASHIRIA HAZIKUWA NA KEMIKALI AU MBOGA MBOGA ZILIZO LEGEA KIDOGO KWAMBA ATA KAMA ZILIKUA NA KEMIKALI BASI SIO KIASI CHA KUTISHA.

NICHUKUE NAFASI HII KUWAALIKA WADAU WOTE WA KILIMO KUJA KUJIFUNZA NA KUKUTANA NA WATAALAMU KUTOKA TANZANIA NA WALE KUTOKA NCHI ZA NJE WATAKAOSHIRIKI KUTUAMBIA NCHINI

KWAO WANAFANYAJE KWENYE HAYA MAMBO. MAJIRANI ZETU – UGANDA WANA SERA YA TAIFA YA KILIMOHAI (NATIONAL ORGANIC AGRICULTURE POLICY). SISI TUKIANZA NA HUU MKAKATI TUTAFIKA PAZURI HUSUSAN KWENYE USALAMA WA CHAKULA, AFYA YA MLAJI, UDONGO NA MAZINGIRA KUPITIA MBINU ZA KILIMO ZA KILIMOHAI.

NIMALIZIE PIA KUWAKARIBISHA PIA TAASISI BINAFSI WALIOWEKEZA KWENYE MASWALA YA KILIMO KUJITOKEZA NA KUDHAMINI KONGAMANO HILI AMBALO TUNATARAJIA NA TUTAWATANGAZIA BAADAE MGENI RASMI KUWA WA NGAZI YA JUU KATIKA TAIFA LETU.